Thursday, July 19, 2012

LUPITA NYONGO AULA HOLLYWOOD

Mwanadada mcheza filamu wa Kenya, Lupita Nyongo ambaye anajulikana sana kupitia MTV shuga Series kama Ayira, amepata deal la kucheza filamu katika jiji la Obama land ndani ya Hollywood, maskani yanayoongoza katika nyanja ya filamu duniani. Lupita amepata deal la kucheza filamu moja pamoja na Kina Brad Pitt kwa kushika nafasi ya Mfungwa mwenye upendo na Ukatili. Kupitia mtandano mmoja ambao umetoa habari hizi.

Lupita atacheza filamu hii pamoja na wacheza filamu wengine maarufu wa Hollywood kama Brad Pitt Brad Pitt, Alfre Woodard, Chiwetel Ejiofor, Ruth Negga, Adepero Oduye, Paul Dano, Benedict Cumberbatch, Scoot McNairy, Garret Dillahunt, Paul Giamatti pamoja na Sarah Paulson. Filamu hii itatengenezwa katika Studio za Plan B Entertaiment zinazomilikiwa na Brad Pitt mwenyewe.

0 Comments: