Thursday, July 19, 2012

BOBY BROWN NAE KAOA?


Hayawi Hayawi .... Robert Barisford "Bobby" Brown" mwandishi wa nyimbo na mwanamuziki wa miondoko ya RnB nchini marekani, ambaye mwaka 2007 walichapana talaka na mke wake wa zamani, Marehemu Whitney Huston, amefunga ndoa na mpenzi wake wa zamani Alicia Etheredge hivi karibuni.

Harusi hiyo ambayo ilihudhuriwa na watoto wake watatu, Landon, 23, La’Princia, 22, na Bobby Jr., 19. Bobby Brown ambaye ndoa yake na Whitney Huston ulidumu kwa takribani miaka 14, hadi kufikia mwishoni ikiwa na misukosuko ya kuandamwa na magazeti na vyombo vya habari kuwa Bobby Brown alikuwa na maisha ya utumiaji madawa ya kulevya, Vurugu na matusi kwa Whitney Huston. Bobby Brown na Alicia Etheredge

waliweka wazi uchumba mwaka 2010 baada ya Bobby Kumaliza show yake iliyofanyika mji wa Jacksonville Floridah.

0 Comments: