MSANII mahiri wa muziki wa regge na ragga nchini Ahmad Suleiman"HardMad" amesema hali tete ya soko la muziki imechangia kushuka kwa kiwango cha sanaa nchini.
Aliyasema hayo alipokuwa akiongea na Burudanikilasiku jijini Dar es salaam jana,alisema kutokana na hali ya soko la muziki nchini kuwa katika hali isiyoeleweka,wasanii wengi wamevunjika moyo kuendelea kutunga vibao.
Hardmad alisema kuwa hali ya soko la muziki ndiyo kichocheo kikubwa cha kuvumbua vibaji vipya kutokana na wasanii wengi kutumia muziki kama ajira ya kuweza kuendesha maisha yao.
"Wengi tunategemea muziki kuweza kuendesha maisha yetu pamoja na masuala mengine,ila kama soko la muziki ni tata ni lazima tutazame upande mwingine kitu ambacho kinachangia muziki kushuka:" alisema msanii huyo.
Hardmad msanii anayetamba na vibao vyake kadhaa vikiwemo Ni wewe,Tamala na vingine kadhaa lisema hali hiyo imechangia kwa kiasi kikkubwa kuwafanya wasanii wengi wakubwa kuwa kimya kwa ssa kutokana na hali ya muziki wenyewe na hasa soko kuwa katika hali ya utata.
Akizungumzia mikakati yake ya sasa alisema ameakamilisha kazi ya kurekodi albamu yake mpya ambayo ni tatu kwake ikiwa imebeba jina la Imebaki stori,ikiwa na vibao kumi na mbili.
"Naongelea kuhusu sanaa ya bongo kwamba sasa imebaki stori tu kwa kuwa hakuna kitu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma" alisema Hardmad.
Alisema tayari video ya kibao kimoja ndani ya labamu hiyo,Ujio mpya imeanza kuonekana na kufanya vizuri katika vituo mbambali vya luninga baada ya kusambaza katika siku za karibuni.
Harmad alisema video hivyo ambayo imerekodiwa na kampuni ya Visual Lab ya jijini Dar es salaam imeshasambazwa katika vituo mbalimbali vya luninga ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya albamu yake hiyo mpya ambayo itakuwa ya tatu.
"Hii ni albamu yangu ya tatu,albamu yangu ya kwanza,Sina Muda,Ni wewe na hii sasa,Imebaki Stori ni albamu yangu ya tatu" alisema msanii huyo.
Pamjoja na hayo aliseam kwa sasa anajipanga kwa kusaka wadhamini kwa nia ya kuitambulisha albamu yake hiyo kwa washabiki wake muda ukifika.
"Napenda kuwaambia washabiki wangu,kimya changu kimekuja na kishindo kikubwa ,nimewashirikisha wasnii wengi wenye vipaji" alisema.
Alisema ndani ya albamu yake hiyo wapo wasanii kadhaa ambao amefanya kazi nao wakiwemo Enika, Phantom,Peace toka Uganda,na wengine wa ndani na nje ya nchi.
Albamu hiyo ambayo imebeba jumla ya vibao 12,imerekodiwa katika studio tofauti zikiwemo 14 records ya jijini Dar es salaam na Jacob Paul Productions ya nchini Denmark kwa lengo la kuleta ladha tofauti.
Publisher: James Nindi
0 Comments:
Post a Comment