MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Danny Msimamo amesema bado yupo imara katika fani na kimya chake kinatokana na masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa masomoni.
Akiongea na burudani kwa njia ya simu toka Korogwe,Tanga jana alisema kwamba amekuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na kuwa na shughuli kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa katika masomo,Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika kitengo cha komputa.
Msanii huyo alisema kutokana na kuwa katika masomo hayo muda wake ulikuwa mdogokiasi cha kutoweza kujigawawa katika yote.
Aidha msanii huyo alisema kwa sasa amekamilisha kazi zake kadhaa mpya na anatarajia kuazitambulisha kwa wshabiki muda muda wowote kuaanzia sasa sambamba na video za vibao hivyo.
"Nilikuwa kimya kwa ajili ya shule pamoja na kusoma mwenendo wa soko la muziki huu ambalo kwa sasa ni tata" alisema msanii huyo ambaye anatamba na vibao vyake kama Mic,Siku nzuri na vingine kadhaa.
Msanii huyo alisema kwa sasa yupo kamili kuanza kutambulisha kazi zake mpya kutokana na muda alikaa kimya kuutumia kufanya utafiti.
"Sijaishiwa,kisanii nakuja ,tena nakuja na nguvu kubwa kabisa nikiwa na tungo za kufa mtu" aligamba.
Aidha msanii huyo alisema ni kweli alikaa kimya kwa muda mrefu akiwa na majukumu mengine likiwemo la kuongeza elimu na pia alikuwa anatumia muda huu kufanya utafiti kuhusu soko la muziki.
"Kukaa kimya ni kutoridhishwa na mwenendo wa soko la muziki huu nchini,lakini sasa nimeamua kuja ili kuwapa ladha washabiki wangu" alisema.
Aidha msanii huyo alisema anakuja na tungo kadhaa kwa ajili ya utambulisho wa kazi zake mpya kwa nia ya kuanza kujitangaza baada ya kimya cha muda mrefu.
Msanii huyu alisema kwa sasa anajipanga kuanza kujitangaza kupitia nyimbo zake hizo mpya sambamba na video zake.
"Sikuwa na video nyingi,sasa nimeamua kufanya na video ili washabiki wangu waweze kupata ladha kamili" alisema.
Akizungumzia hali ya muziki huo nchini kwa sasa,alisema pamoja na wasanii wengi kufanya kazi nzuri,bado wasambazaji na wadau wengine wanasimamia kazi za wasanii wanashindwa kufanya kazi zao kwa kwa uaminifu.
"Hali ya soko la muziki nchini,iko tete,na hii ikiendelea wasanii wengi wazuri tutawapoteza" alisema msanii huyo.
Pamoja na hayo,msanii huyu alishauri wasanii kuwa na umoja kwa nia ya kudai haki zao kwa pamoja kwa kuwa umoja utaongeza nguvu miongoni mwao.
Story:James Nindi
Tuesday, July 20, 2010
Sio kimya bali masomo ndio yanabana-Danny Msimamo
Tuesday, July 20, 2010
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment