KUNDI la muziki wa Kikosi cha Mizinga yenye maskani yake kinondoni jijini Dar es Salaam limewataka wasanii mbalimbali kutumia studio yake kwa kuwa ina lenga kuwasaidia wasanii wote.
Akichonga na burudanikilasiku, jijini Dar ers salaam hivi karibuni,Kiongozi wa kundi hilo,Masoud Karama a.k.a Kallapina alisema kundi lake limeanzaisha studio hiyo kwa ajili ya kusaidia kuendeleza muziki kwa wasnii wote.
Alisema kutokana na hilo ni vema wasnii na wadau mbalimbali wa amasuala ya muziki kuitumia studiio hiyo kwa nia ya kujiendeleza kimuziki.
"Studio yetu ni ukombozi kwa wasanii wote,hivyo haijaanza kwa nia ya kurekodi tungo zetu sisi tu" alisema msanii huyo.
Aidha msanii huyo alisema kwa sasa kundi lake limeongeza vifaa kadhaa vipya kwa nia ya kuboresha utendaji wa kazi ndani ya studio hiyo na wasanii mbalimbali ndani na nje ya jijini Dar es salaam wamefika kuitumia.
"Hii ni studio ya wasanii wote,hivyo naomba tuitumie kwa kuendeleza muziki wetu hapa nchini" alisema.
Akizungumzia mikakati ya kundi lake kwa sasa,alisema kundi lake limejipanga ufanya mambo makubwa katika kipindi hichi ikiwa ni pamoja na utambulisho wa kazi zake mpya sambamba na filamu.
"Bado tupo katika mazungumzo na watu mbalimbali,ila tunahitaji wadhamini waje kutuunga mkono katika mikakati ya uzidunzi wa albamu yetu mpya" alisema Kiongozi huyo bila kutaka kuingia ndani zaidi.
Akizunguzia hali ya mnuziki huyo nchini kwa sasa,alisema hiphop kwa sasa inapenda na idadi ya wahabiki wake imeongezeka kitu ambacho ni ishara nzuri kwa muziki huo na wasanii wake.
"Zamani washabiki walikuwa wahatuelewi,ila sasa wametuelewa na hilo limetokana na mchango mkubwa tulioupata kupitia vyombo bvya habari,kweli tunavipongeza kwa kazi nzuri kwetu" alisema.
Publisher: James Nindi
0 Comments:
Post a Comment