MSANII wa muziki wa kizazi kipya Gerald Simba a.k.a Ras Lion amesema kimya chao cha muda mrefu na swahiba wake Michael Muhina a.k.a John Woka kinatokana na kuwa katika maandalizi ya kazi zao mpya.
Akichonga na burudanikilasiku,jijini Dar es Salaam,alisema wamekuwa kimya kwa muda mrefu wakifanya utafiti na kuona ni jinsi gani muziki huo unataka.
Alisema wamekuwa katika utafiti kwa muda mrefu na baada ya utafiti wao huo wameona na kutambua mamtaizo mengi ya kijamii ambayo yanahitaji ufumbuzi wao kupitia muziki.
"Tulikuwa kimya sana tukifanya utafiti ,.utafiti ambao ulitupelekea kusafiri sehemu tofauti,kuongea na watu na sasa,tumekuja na kazi ambazo zinatokana na utafiti wetu" alisema Ras Lion.
Msanii huyo alisema kwa sasa wamekuja na vibao kadhaa vipya vikiwa vimebaba ujumbe mabalimbali kwa nia ya kuelimisha jamii na hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu.
"Kuna kibao kinaitwa Babu,ndani ya babu tunaongelea wosia wa hayati Mwalimu Nyerere,hivyo wananchi watapata kusikia kazi hii ndani ya albamu yetu mpya, Sumu ya Panya iliyopo sokoni"alisema.
Ras Lion alisema ndani ya albamu hiyo ambayo wamefanya kwa kushirikiana na shwahiba wake John Woka imeshaingia sokoni ikiwa na idadi ya nyimbo kumi na tano na imerekodiwa katika studio za n Grandm,aster,Arusha pamoja na studio za Sound Crafters,Darc es salaam.
"Tumetumia studio tiofauti ili kuleta ladha tofauti ya kimuziki kwa washabiki wetu" alisema Ras Lion.
Aidha msanii huyo alisema baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi albamu hiyo,kwa sasa wanajipanga kuendelea na kazi ya kurekodi video za albamu yao hiyo.
"Hatujaacha muziki,tulikuwa na kazi ya utafiti na sasa,washabiki wetu wataweza kutusikia"alisema msanii huyo ambaye alihi kutamba na vibao vyake kadhaa kikiwemo Umasikini Huu.
Akizungumzai hali ya muziki huo nchini kwa sasa,alisema muziki unakwenda vizuri ila bado wizi ni mkubwa kwa kazi za wasanii kitu ambacho kinapelekea wasanii kushindwa kufaidi matunda yao vema.
Story:James Nindi
Tuesday, July 20, 2010
Tupo katika utafiti kwa sasa- Ras Lion na John Woka
Tuesday, July 20, 2010
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment