Sugu
MB Dog
Kile chama cha muziki wa kizazi kipya cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) kilichokuwepo mwanzo na kupotea sasa kimerudi kwa nguvu zote kikiwa na dhumuni la kutetea kazi za wasanii wenyewe.
Chama hicho kinachowaunganisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya kina lengo la kukuza la kuendeleza muziki wa Tanzania na kujenga kitu kimoja sasa kimerudoi baada ya kupotea kwa muda na kutokuwa na nguvu ya pamoja ila kwa sasa kimerudi upya kikiwa na lengo moja la kumtetetea haki ya msanii.
Baadhi ya wasanii waliokuwepo katika kikao hicho wamesema wameamua kuja kwa nguvu moja ili kutetea kazi zao na kujua kitu gani wanatakiwa kukifanya kuhusiana na muziki wanaoufanya na kuacha kunyanyaswa na baadhi ya watu wasiokuwa na uchungu na muziki wa kizazi kipya.
Chama hicho cha TUMA kilichokutana leo jumamosi mida ya saa 4:00 asubuhi na kufanya mkutano wake Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) jijini Dar es Salam kikiwa lengo la kuendeleza muziki wa Tanzani ili kufikia levo ya kimataifa kiliudhuliwa na wasanii mbalimbali kama vile Mkoloni, Braton, Rado, Sugu, John Mtambo, Dotto wa mapacha, Mb Dog, Yakuza Mobb, . G-Sollo na wengine wengi.
Mada zilizochangiwa na wajumbe waliokuwepo katika kikao hicho ni juu ya kukiendeleza chama hicho na kuwa na misingi na katiba kisheria ili kiweze kuwatetea wasanii kwa .
Katika kikao hicho kilichofanyika BASATA nilipendekeza kuundwa kwa kamati ya muda kwa ajili ya kufuatilia mwenendo mzima wa kukiendeleza chama hicho ili kifike na kiweze kuuendeleza muziki wa Tanzania. Baadhi ya wajumbe waliochaguliwa katika kikao hicho kama viongozi wa muda ni pamoja na MB Dog, Mkoloni, Sugu, G-solo, Doto wa Mapacha, Braton, Rado, Mr O, Stara Thomas na Azma.
Mimi kama mmoja wa wajumbe waliokuwepo katika kikao hicho nimefurahishwa sana kuona wasanii wanakuwa na umoja kama huo ili kuachana na ile dhana kwamba hawawezi kufanya kazi zao wenyewe na kuwategemea watu wengine ambao hawana uchungu na muziki wa Tanzania .
Kwa kumalizia napenda kuwapa pongezi wasanii walioamua kupambana na kazi zao wenyewe na sisi kama wadau tunaopenda kuona muziki unaendelea na kufikia levo ya kimataifa tuko nao pamoja mwanzo mwisho pia watanzania wengine wenye nia na kuwapa moyo wasanii wetu wa nyumbani tunaomba kuwaunga mkono ili kukiendeleza chama chetu cha Tanzani Urban Music Association (TUMA) kifike mbali ili baadae kije kuwanufaisha wasanii wetu wa nyumbani.
Mengi kuhusiana na TUMA endelea kufuatilia blog yako ya burudanikilasiku
Saturday, March 13, 2010
Tanzania Urban Music Association (TUMA) yarudi kwa kishindo.
Saturday, March 13, 2010
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments:
Post a Comment