Friday, February 5, 2010

Cindy aja na kitu kipya “One and Only”

Baada ya kujiengua katika kundi la Blu3 mwanadada, Cindy walimwambia hatafika mbali kutokana na kujitoa kwake lakini kwa sasa ameuziilishia uma kwamba anaweza na sasa amekuja na kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la “One and Only”.

Wimbo huo umetengenezwa kwa kutumia biti ya Kijamaika na mashairi yake ameyafanya katika lugha ya Kiingereza na Luganda lugha ya kiganda. Cindy ambaye mkali ya dance-floor, amesema nyimbo hiyo itawashika mashabiki wake kutokana na kuwa na ladha mbalimbali ndani yake.

Mwanadada huyo amesema wimbo huo ni maalumu kwa watu wote ambao hupenda kuwa na wapenzi wengi na kuacha kuwa na mpenzi mmoja na kuwa na wapenzi wengi na kuwasihi kuachana na tamaa na kusababisha kutokuelewana kwa wapenzi.

Alimalizia kwa kusema kuwa “Sasa ni wakati wa kungalia soko la muziki linaendaje ili kuangalia vipaji vya wasanii wengine na kuachana na malumbano kama yeye alivyojiengua kundi la Blu 3 kulivyokuwa na malumbano yasio na msingi ila kwa sasa mambo kama hayo hakuna tena, kwani huu ni wakati wa kungalia nini unafanya,”alisema Cindy.

0 Comments: