Wednesday, December 30, 2009

Wayre amaamua kuoa

Wayre, Nazizi na Bebe cool wakifanya makamuzi

Ebwana eeh! unajua kama mwanamuziki Wayre anayeunda kundi moja la Necessary Noize, Nazizi na Bebe Cool wa Kenya kwa sasa ameamua kuoa na kuachana usemi wa Mwana FA wa kuwepo kuwepo.Msanii huyo amesema ndoa yake ni nzuri na kuwashauri wengine kufuata njia kama yake ya kuoa.

Msanii huyo ambaye ni mcheshi na kila mtu amesema aliamua kufanya hivyo baada ya kuona muda umefika wa kufanya hivyo umefika.

Wayre amesema baada ya kuoa kwa sasa yuko katika maandalizi ya albamu ya pili kama solo artist na itakuwa katika maadhi ya R&B baada ya ile ya Dancehall kama mashabiki wake wanavyomjua, na hii ameamua kufanya hiyvo ili kuangalia muelekeo wa muziki unavyoenda.

“Nimeamua kufanya hivyo baada ya kuona baadhi ya wasanii wengi wa Kenya kupenda kufanya muziki wa R&B na siwezi kufanya Dancehall kwa sasa kama navyofanyaga kwani nataka kuangalia nafanya kitu kipya.

Msanii huyo nilimuuliza kuhusiana na kundi la Necessary Noize alisema kundi lipo na linaendelea kuwepo ila kwa sasa msanii mwenzake Nazizi yupo bize na albamu yake kama anavyofanya yeye ila kila mtu akishakamalisha ‘project’ yake watafanya kazi kama Necessary Noize.

Wayre amesema kwa sasa muziki anaangalia kimataifa zaidi na kwamba anafikiria kufanya muziki na wasanii wa kimataifa zaidi ili kukuza muziki wake kufika levo ya kimataifa na kuongeza kuwa atafanya muziki na wasanii wa kimataifa ili kuangalia unaweza kufanya vizuri zaidi.

Alimalizia kwa kuwaasa wasanii wenzake kuwa na juhudi ya kuufikisha muziki wa Afrika katika levo ya kimataifa ili kuleta mapinduzi baada ya kukaa na kufikiria kufanya muziki ambao hayatasaidia muziki kufika mbali.

0 Comments: