Wednesday, December 30, 2009

Nyota ndogo aamua kuimba Kiingereza

Nyota ndogo akiwapagawisha mashabiki wake

Sio jina geni masikioni mwa wapenzi wa muziki wake hapa na nchini Kenya, hapa namzungumzia Nyota ndogo ambaye kwa sasa muziki wake amuamua kuuimba katika lugha ya kiingereza.

Msanii huyo aliyetamba na kibao chake cha Watu na viatu kipindi cha nyuma alichonga nasi na kusema kuwa aliamua kuingia darasani ili kujifunza zaidi kiingereza ili kupata ujuzi ili afanye muziki wake katika levo ya kimataifa zaidi.

Wimbo alioufanya katika lugha ya kiingereza umekwenda kwa jina la I’m Gonna be Fine ambao amemshirikisha mwanamuziki kutoka Malawi anayekwenda kwa jina la Tay Grin.

Mwanadada huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja anayekwenda kwa jina la Mbarak amesema ameamua kufanya hiyo baada ya kukaa darasani akisoma lugha hiyo vizuri ya kiingereza ili kuweza kukimbizana na wasanii wa kimataifa.

Mwanadada huyo kwa sasa yuko katika maandalizi ya albamu yake mpya ambayo bado hajaipa jina na kwamba itakuwa katika lugha mbili ambayo ni kiingereza na kiswahili ili kuleta ladha tofauti kwa wapenzi wake wa muziki wa Afrika mashariki na duniani kwa ujumla.

0 Comments: