Wednesday, December 30, 2009

AY aja na Kings and Queens

Ambwene Yessaya na Jokate katika video ya KINGS AND QUEENS
Ambwene Yessaya katika pozi
Hii itakuwa imetulia zaidi kwa kuumaliza mwaka kwa msanii Ambwene Yessaya ‘AY’ kwa kudondosha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la KINGS AND QUEENS aliyowashirikisha wanadada JOKATE na AMANI kutoka KENYA.

Wimbo huo umetayarishwa na Super Produza HERMY B kutoka ndani ya Studio ya B.Hitz Music Group na video yake inafanywa na OGOPA DEE JAYS toka Kenya na Video hiyo mpaka sasa imeshafanya ndani ya Jijini Nairobi na itaanza kuruka hewani wiki ijayo MTV BASE huku vituo vingine ndani ya Afrika Mashariki itafuata.

Katika wimbo huo Ambwene amejaribu kufikisha fikra zake kwa mashabiki ya kwamba MWANAMKE WA KIAFRIKA NDIE BORA KABISA NA ANAJISIKIA FAHARI SANA KUZALIWA NDANI YA BARA HILO LA AFRIKA.

Alimaliza kwa kusema kuwa kwa mwaka 2010 ni mwaka ambao ni wa mapinduzi kwa wasanii wa Afrika mashariki ambapo mzee wa COMMERCIAL amewataka mashabiki wake wasubiri mambo makubwa kutoka kwake kwani ameamua kuiwakilisha vilivyo Afrika Mashariki katika anga mbalimbali ya muziki.

0 Comments: