Wednesday, December 30, 2009

Bobi Wine apewa jukumu la kuwaelimishaa wavuta Bangi

Bobi wine akifanya mazoezi nyumbani kwake.

Msanii Bobi Wine wa Uganda ambaye kwa sasa ndio anaongoza kuwa na kipato kikubwa kwa wasanii wa Uganda akifuatiwa na Chameleone amepewa jukumu la kuwasimamia wavuta bangi na wabwia unga wote nchini Uganda.

Bobi Wine ndio kiongozi wa kuwaongoza na kuwasihi watumiaji wa vitu hivyo kuachana navyo ambapo na yeye amesema kuwa kazi hiyo ni ngumu kwake ila atajitaidi kukabiliana nayo kwani yeye mwenyewe ana shamba la bangi nyumbani kwake.

Kutokana na kuwa na wakati mgumu kukabiliana na suala hiyo msanii huyo ameahidiwa kupewa ushirikiano na hao waliompa kazi hiyo ili kuwaepusha baadhi ya vijana waliojiingiza katika janga hilo la kutumia madawa ya kulevya na bangi.

0 Comments: