Thursday, December 31, 2009

Ng'ang'a akamilisha albamu yake ya Zawadi

Mkubwa hii inaweza kuwa kama utani vile, lakini ndio ukweli wenyewe ambapo mshiriki aliyekuwa anapingwa vikali na majaji katika shindano la Tusker Project Fame III, Bernard Ng'ang'a au Ng'ang'alito ameachia albamu yake mpya.

Mshiriki huyo aliyekuwa anapigwa na majaji katika shindano hilo ya kwamba hana kipaji amewafunika washiriki wenzake kwa kuachia albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Zawadi.

katika albamu hiyo ambayo amesema ina nyimbo tisa na imeshakamilika na kilichobaki kwa sasa ni kuipeleka kwa mashabiki wake na ndani ya albamu hiyo ameimba katika lugha ya Kikuyu, Kiingereza na Kiswahili.

Ng'ang'a alitudokeza kuwa katika kufanya albamu yake hiyo ni kwasababu ya kuwa na moyo wa kujituma kwani anasema kuwa " Lilipoisha shindano la Tusker Project Fame nilikuwa na kibarua kizito cha kujifungia ndani na kuandaa albamu hii na nimefurahi sana kukamilisha albamu yangu ya Zawadi", alisema Ng'ang'a.

0 Comments: