Thursday, December 31, 2009

Bracket kufanya makamuzi ndani ya jiji la Nairobi


Hii itakuwa imesimama zaidi kwa wakazi wa Nairobi kwa kuufunga mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka 2010 kwa kufanyika bonge la tamasha ambalo litaporomoshwa na kundi la Bracket la nchini Nigeria linalotamba na kibao chao cha Yori Yori.

Katika tamasha hilo litakalofanyika siku ya tarehe 2 januari 2010 katika ukumbi wa Carnivore mida ya saa moja usiku na kusindikizwa na wasanii wa nchini humu ambao ni pamoja na Habiba, Nameless na Nonini kiongozi wa Genge ili kuwapa mashabiki kitu roho inapenda.

Kundi hilo la Bracket linalotamba na vibao vyao vikali vya "Yori Yori" na "No time" walivyoshirikiana na kundi la P-Square linatarajia kuingia nchini Kenya muda wowote kuanzia sasa ambapo kampuni ya Palm Springs Entertainment inayowaleta imesema kuwa limeshakamilisha kila kitu kuhusiana na tamasha hilo.

0 Comments: