Nyota huyo alifunguka hayo alipoulizwa swali kuhusu uhusiano wake na nyota huyo ambapo aliongeza kuwa Vanessa Mdee kwake kwanza ni familia yake halafu anafuata yeye.
“Nampenda Vanessa kuliko msichana yeyote yule na sitegemei kumuacha, hata familia yangu inajua kuwa nina upendo mkubwa kwa Vanessa.
“Nikiwa mbali na Vanessa nikiamka asubuhi cha kwanza naingiaga Instagram kumuangalia baada ya hapo ndo nampigia simu siwezi, kumpigia simu bila kuangalia picha zake. Kiufupi nampenda sana Vanessa,” alisema Jux.
“Saíhivi natamani kupata mtoto na nina mpango huo kwa sasa wa kujipanga kupata mtoto na mpenzi wangu pia mtoto wangu wa kwanza nataka nimuite jina la Karim na si jina jingine zaidi ya hilo”.
0 Comments:
Post a Comment