Saturday, September 9, 2017

Lady Jaydee kumwaga fedha kwa Instagram

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameamua kumwaga fedha kwa mashabiki kupitia mitandao ya kijamii kwa kuanzisha shindano katika ukurasa wake wa kijamii ‘Instagram’.

Shindano hilo linahusisha maswali na endapo washindi watatu watakaoweza kujibu kwa ufasaha maswali matatu atayatoa kwenye mtandao huo watalamba jumla ya sh. milioni 2.
Lady Jaydee alisema katika mashindano hayo mshindi wa kwanza atajipatia milioni moja huku mshindi wa pili akipata laki saba na nusu na mshindi wa tatu atapata laki mbili na nusu ambapo kwa jumla atakuwa ametoa sh. milioni mbili kwa washindi wote watatu.
Lady Jaydee ambaye sasa yupo katika kampeni ambayo baadhi ya mashabiki wake wamekuwa wakihisi huenda ni ujio mpya wa kazi yake mpya, huku wengine wakihisi huenda kuna jambo jingine mwanadada huyo anataka kufanya, lakini kwa mujibu wa historia Lady Jaydee amekuwa akifanya kampeni mara kadhaa pindi anapokuwa anaachia kazi zake za muziki.

0 Comments: