Saturday, September 2, 2017

Dogo Janja, Irene Uwoya ni washikaji tu


MSANII Dogo Janja amejibu swali ambalo kwa muda mrefu watu wamekuwa wakijiuliza hasa baada ya kuonekana kuwa karibu na msanii Irene Uwoya kiasi cha kudaiwa kuwa wawili hao wapo kwenye dimbwi la uhusiano wa kimapenzi.
Akizungumza wiki hii, Dogo Janja amesema kuwa Irene si mpenzi wake na hawajafikiria kuwa na uhusiano naye lakini ukweli kutoka kwenye moyo wake anampenda.
“Ukaribu wangu na Irene Uwoya ni wa kawaida tu na hakuna kilichokuwa kinaendelea kati yetu ingawa watu wameuchukulia tofauti na uhalisia. Nampenda sana yule dada lakini kuwa na mazoea naye kidogo kumezua maneno mengi,”anasema.

0 Comments: