Akizungumza juzi, Amini anayetamba na wimbo wake mpya wa Yamoyoni , anasema taarifa za kujifungua kwa Linah alizipata na alichokifanya alimuombea tu kwa Mungu lakini ameshindwa kumpa zawadi.
Anasisitiza hadi sasa hajampongeza wala kumpelekea zawadi kwa sababu hajui anakaa wapi na wala hana namba zake za simu.
“Nilipojisikia amejifungua mtoto wa kike nikasema Mwenyenzi Mungu amfanyie wepesi na mtoto wake na waishi vizuri katika maisha yao,”anasema.
Amin anasema anatambua namna ambavyo Linah alikuwa anatamani kupata mtoto na sasa amebahatika kumpata.
0 Comments:
Post a Comment