MUIGIZAJI wa filamu za kibongo Shamsa Ford amewabwatukia baadhi ya wanaume wenye tabia ya kupenda kulelewa na wanawake.
Shamsa amesema hayo kwa kuandika kwenye mtandao wa Instagram ambapo anaonesha kukerwa na tabia hiyo ya wanaume wanaotaka wawe tegemezi kwa wapenzi wao na ukifuatilia utabaini wapo hivyo kwasababu ya kuchagua kazi ya kufanya.
Anafafanua kuwa “Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume niwashauri jitumeni kwa kufanya kazi kwa bidii. Usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini.
“Mwanaume unatakiwa kupambana na maisha , fanya kazi hata ya kusukuma mkokoteni kikubwa ni kupata fedha ya kujikimu kimaisha.”
Akatumia mtandao wake kuwabwatukia wanaume wenye kujiona wana sura nzuri na matokeo yake wapo tayari kulelewa na wanawake wenye fedha.
“Wanaume wenye tabia hiyo hamuoni aibu maana mnaitwa kila majina mpo.Utasikia mara mnaitwa vichura, vibenten,vipanyabuku,vitom and jerrydaah”.
Anaongeza huu ni wakati wa kufanya kazi, hivyo wanaume wenye tabia ya kuchagua kazi waache kwani haitawasaidia katika maisha yao.

0 Comments:
Post a Comment