Saturday, August 26, 2017

Nay awatolea uvuvi Kiba, Diamond, Dimpoz


MSANII maarufu Emmanuel Eribarick ‘Nay wa Mitego’amewashauri wasanii Ali Kiba, Ommy Dimpoz na Diamond kuacha tabia ambayo wanaifanya mitandaoni ya kushambuliana na kuhusisha wazazi kwenye malumbano yao.
Kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii kuna vita badiri inayoendelea kwa wasanii hao watatu, hata hivyo vijembe ambavyo vimefikia hatua ya kuhusisha wazazi, ndio imemfanya Nay wa Mitego kuibuka na kuonya tabia hiyo.
Nay anawataka wasanii hao wagombane na ikiwezekana hata kurogana mpaka wauane lakini si kuingiza wao kwenye makumbano yao.”Tukananeni matusi yote wenyewe kwa wenyewe ikibidi piganeni kabisa atakaye kufa tutazika na itakuwa historia kama Big na Pac.
“Taibia ya kuingiza wazazi ni ujinga na sipo tayari kuona ukiendelea.Sipo upande wowote si kwa Kiba, Dimpoz wala Diamond, endeleeni na vita yenu kama wanawake mmechukuliana mabwana, ila suala la wazazi mnavuka mipaka,”anasema kupitia mtandao wa Instagram.

0 Comments: