Saturday, August 26, 2017

Mziwanda aleta Bao la ushindi

MSANII Nuh Mziwanda amefafanua maana kamili ya wimbo wake mpua wa Bao la Ushindi.
Akizungumza juzi Nuh ambaye alikuwa kimya kwenye muziki tangu alipoachana na mkewe na sasa amekuja na wimbo huo mpya.
Anafafanua wimbo huo unazungumzia mafanikio ambayo mtu huyapata kutokana na utafutaji wa kila siku na kuongeza Bao la Ushindi hauhusiani na mambo ya mapenzi bali unahusu ushindi.
“Hapa maana yangu ni kwamba ni ushindi wa kila kitu kwenye maisha, ni ushindi katika kupata fedha , kupata dili au kufurahia jambo.Mfano naweza kuzungumzia kupata mtoto na mtu yeyote atasiliza,”anasema.

0 Comments: