Saturday, August 26, 2017

Mercy Johnson apewa heshima ya kipekee

MSAIDIZI Mkuu wa Gavana wa Serikali ya Kogi katika masuala ya burudani, sanaa na utamaduni, Mercy Johnson Okojie, amepewa heshima ya kipekee alipokwenda kutembelea katika jimbo hilo.
Msanii huyo mkongwe wa Nollywood, alipewa kasi maalumu ya kusaka vipaji katika jimbo hilo, hivyo alikwenda kumuona kiongozi wake ili kumpa sapoti.
Mdhamini kutoka ardhi ya watu wa Okun, HRH Oba Michael Yusuph alimpa heshima kubwa wakati akimkaribisha mkongwe huyo akiwa na timu yake jimboni kwake.
Mercy pamoja na timu yake waliingia katika jumba hilo, kumtaarifu mdhamini huyo kutoa sapoti na baraka katika mpango wake wa kuinua vipaji.
“Najua unakwenda kutafuta vipaji na nina uhakika utavipata na upo katika mikono salama.Watu wako wanaweza kuja hapa kupiga picha za video kwakuwa kuna vitu vingi hapa kama Obangogo.Hatuchezi na mwanamke ila kitu kitu tumekuachia wewe,” alisema Yusuph.

0 Comments: