Saturday, August 19, 2017

Kumbe jina la Barakah Da Prince lilitolewa na Dully

MSANII wa  Bongo Flava, Prince Dully Sykes, amesema msanii wa muziki anayemiliki lebo ya Bana, Barakah The Prince anamwita baba katika muziki.
Dully ametoa kauli hiyo baada ya kueleza Barakah The Prince anamuita baba na Young Dee anamuita babu katika muziki.
“Nilimpa jina la Da Prince jina ambalo limeishia na mimi, Baraka ananiita Baba na Young Dee ananiita babu kwa kuwa aliletwa na mwanangu Mr. Blue,”anasema Dully.
Kwa sasa unapozungumzia msanii mkongwe kwenye muziki huo basi jina la Dully haliwezi kukosekana na hiyo imemfanya aheshimiwe na wasanii wenzake.

0 Comments: