Tuesday, August 15, 2017

Jim Iyke aunga mkono maandamano ya Buhari

MSANII nyota wa Nigeria, Jim Iyke ameungana na wananchi wengine nchini humo kufanya maandamano juu ya Rais wao, Muhammadu Buhari katika maeneo ya Abuja.
Rais Buhari yupo nje ya nchi hiyo kwa siku 90 sasa akipatiwa matibabu wa ugonjwa ambao haujawekwa wazi na wanamtaka aje aendelee na kazi au ajiuzulu.
Waandamanaji hao wanaongozwa na Fada Charles Oputa, yamekuwa yakiendelea kwa muda sasa.
Wasanii wa fani mbalimbali wamezidi kuunga mkono suala hilo moja kwa moja na wengine kwa kujificha.
Miongoni mwao ni Jim Iyke ambaye alisema;”Ni kitu kidogo sana, tunamuomba rais wetu aje kuendelea na kazi au ajiuzulu”.

0 Comments: