Tuesday, August 22, 2017

Genevieve Nnaji amfuata Ronaldo Ureno

NYOTA wa kike wa Nollywood, Genevieve Nnaji yupo jijini Lisbon, Ureno kwa mapumziko na inaonekana anakula bata isivyo kawaida.
Mji huo ndio anaopenda kukaa mwanasoka bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo anayekipiga Real Madrid ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tano kwa kumsukumiza mwamuzi.
Mwanadada huyo alitwaa tuzo ya Msanii Bora wa Kike ya Uongozi na Wajibu 2015 inayotolewa na ‘Africa Movie Academy’, akiwa ndiye msanii wa kwanza wa kike kutwaa tuzo hiyo.
Mwaka 2011, alipewa heshima ya kuwa Mjumbe wa Jamhuri ya Shirikisho la serikali ya Nigeria kutokana na mchango wake katika tasnia ya filamu nchini humo.
Mwanadada huyo ambaye pia ni muimbaji, aliwahi kutamba na filamu kama Road to Yesterday, The Trust with Olisa, Doctor Bello na Half of a yellow sun.

0 Comments: