Tuesday, August 22, 2017

Angela anusurika kuuwawa katika ‘birthday’ yake

MSANII nyota wa filamu za Nollywood, Angela Okorie ambaye katikati ya wiki alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, amenusurika kupigwa risasi na majambazi waliokuwa na silaha siku hiyo hiyo.
Kwa mujibu wa msani huyo, tukio hilo lilitokea wakati akiwa anaendesha gari akitoka katika kituo cha watoto yatima.
Mwanadada huyo alitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wak wa Instagram akiandika;
ìMungu aliye juu hakutaka nifariki, ikiwa ni siku yangu ya kuzaliwa, nimenusurika kupigwa risasi na majambazi ikiwa zimepita dakika 30 nikiwa naendesha gari, hivi kwanini nisiendelee kufanya ibada, ahsante Yesu kwa kuokoa maisha yangu, hakika wewe ni mwema.

0 Comments: