Saturday, July 15, 2017

Ray C kufanya makubwa katika muziki

MSANII mwenye umaarufu wake Rehema Chalamila a.k.a Ray C ameamua kuonesha jitihada zake katika muziki ambapo kwa sasa anatamba na wimbo wake  mpya wa Unanimaliza.
Waanomsimamia msanii huyo katika shuguli zake za muziki wanasema kuwa Ray C ameamua kuonesha kuwa amerudi kwenye game kiasi cha kwamba yupo tayari kukesha studio ili kufanya kazi.
Inaelezwa kuwa tangu alipoamua kurejea kwenye muziki Ray C anataka kuthibitisha kwa mashabiki wake kuwa anataka kurejea kwenye ubora wake wa zamani na katu hayupo tayari kurudi kwenye maisha ya  siku za karibuni ambapo alikuwa kimya  kwenye mambo ya muziki.

0 Comments: