MSANII nyota wa filamu za Nollywood, Omotola Jalade amesema katika maisha yake ya ndoa miaka 21 anajutia dhambi ya uzinzi pekee.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Broadway TV, Omotola alisema dhambi pekee ambayo anajua hatokuja kusamehewa ni kutokuwa mwaminifu katika ndoa yake.
Omotola ambaye ni mama wa watoto wanne, aliweka wazi hilo wakati alipokuwa akizungumzia masuala ya uaminifu ndani ya ndoa.
Alisema mumewe pekee ndiye anayeweza kujua uchungu wa kutokuwa mwaminifu ndani ya ndoa yake na kwamba ni dhambi mbaya.
“Kila uhusiano ni wa kipekee. Je, unaweza kumsamehe mtu asiye mwaminifu? Naweza kusema ndio kama ni mara ya kwanza kufanya na hilo hutokea kama anaonekana kuonesha dalili za kubadilika,” alisema katika mahojiano.

0 Comments:
Post a Comment