BILA ubishi wowote kwa sasa ni wazi lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na Diamond Platnumz ndiyo lebo pekee ambayo inafanya vizuri zaidi katika muziki wa Bongo Fleva.
Ikiwa na takribani miaka miwili sasa, imeweza kusimamia wasanii wa wanne ambao ni Harmonize, Rich Mavoko, Queen Darling ,Rayvanny pamoja na Diamond mwenyewe.
Kitu cha pekee katika lebo hiyo ni ushirikiano mkubwa walionao wa kikazi. Leo kupitia Zeze Kolabo napenda kukuonesha ni jinsi gani WCB wanabebana linapokuja suala la kufanya muziki.
Diamond kaanza kuwabeba
Harmonize ndiye msanii wa kwanza kusainiwa na lebo hiyo na kutoa wimbo wa ‘Iyola’ ambao ndio ulimtoa katika Bongo Fleva. Wakati bado watu wanahoji juu ya uwezo wake, akaamua kumpa shavu bosi wake (Diamond) katika wimbo uitwao ‘Bado’.
Wimbo huo ulitoka mwaka jana mwanzoni na kufanya vizuri zaidi na ninaweza kusema ni wimbo namba moja kwake kwani hakuna wimbo ambao amekwishautoa na kufikia mafanikio hayo.
Ebu chukua huu mfano mdogo, katika mtandao wa YouTube wimbo huu hadi sasa umeshatazamwa na watu zaidi ya milioni 13, wakati ule wa mwanzo ‘Iyola’ ukiambulia watazamaji zaidi ya milioni sita. Hii inaonesha ni kwa namna gani kolabo za Diamond dhidi ya wasanii wake ndani ya WCB zilivyo na nguvu.
Baada ya Harmonize kutoka na kujulikana WCB walimsaini Rayvanny ambaye awali alikuwa chini ya usimamizi wa Tip Top Connection lakini hakufanikiwa kutoka na wakati huo alikuwa anafanya muzuki wa rap na si kuimba kama ilivyo sasa.
Ngoma yake ya kwanza kutoa ndani ya WCB ilijukana kama 'kwetu', ukiwa ni wimbo wake wa kwanza kuimba lakini uliweza kumtoa na kumpa jina kubwa.
Baada ya kuja kufanya vizuri na wimbo wake ‘Natafuta Kiki’, nae alipata nafasi ya kutoa wimbo na Diamond Platnumz lakini hakuwa wake kama ilivyokuwa kwa Harmonize. Wimbo huo uliojulikana kama ‘Salome’ ulimtangaza sana Rayvanny barani Afrika.
Mwaka jana Rayvanny alihusishwa kuwania tuzo za MTV Base, na mwaka huu ametajwa tena na kituo hicho cha runinga kama msanii wa kuangalia zaidi kwa mwaka huu, bila kumasahau Ben Pol.
Msanii wa mwisho kusainiwa na WCB ni Rich Mavoko ambaye kabla ya hapo alikuwa anasimamiwa na lebo ya Kaka Empire kutoka nchini Kenya. Wimbo wa kwanza kutoa katika lebo hiyo ulijulikana kama ‘Ibaki Stori’ ambao ulimrudisha Rich Mavoko ambaye ushawishi wake ulianza kupungua katika Bongo Fleva.
Kama ilivyokuwa kwa Harmonize, baada ya wimbo wa kwanza naye alimpa shavu Diamond katika wimbo wake uliojulikana kama ‘Kokoro’ uliotoka mwishoni mwa mwaka jana na hadi sasa unafanya vizuri. Kwa ufupi ndivyo naweza kusema jinsi Diamond alivyoamua kuwabeba wasanii katika lebo yake kupitia kolabo. Ukimtoa Diamond utangundua wasanii wa chini yake pia nao wanafanya hivyo, ebu tazama.
Queen Darling na Rayvanny
Wawili hawa mwishoni mwa mwaka jana walitoa wimbo ujulikanao kama Kijuso, wimbo ukiwa wa Queen Darling akimpa shavu Rayvanny.
Queen Darling ni msanii wa muda kidogo ambaye alishatamba na nyimbo kama ‘Wajua’ aliyomshirikisha Alikiba, Maneno Maneno aliyofanya na Dully Sykes, na Acha Kokoro.
Aliingia WCB kutokana undugu wa kifamilia alionao na Diamond lakini si sababu ya yeye kubweta kwani kazi yake ya kwanza (Kijuso) ndani ya lebo hiyo matunda yake yanaonekana.
Harmonize na Rich Mavoko
Kolabo ya wawili hawa ndio haswa imenipa ujanja wa kuandika makala haya, wakati picha za kutengeneza video ya wimbo wao zinasambaa mtandaoni wengi walisema WCB wanakuja na wimbo wa lebo nzima.
Binafsi na mimi niliamini katika hilo kwani ‘mbeleko’ ya Diamond ilikuwa imeshamaliza wote ndani ya lebo, sasa ni kipi kingefuata kama si hivyo? Lakini hapa hatukuwa sahihi kufikiri hivyo kwani hawa WCB wanabebana wenyewe kwa wenyewe.
Ndiyo, wanabebana. Ndio maana wiki iliyopita Harmonize kampa shavu Rich Mavoko katika ngoma yake mpya 'Show Me' ambayo imenza kushika kasi mtaani, mtandaoni na katika vyombo vya habari.
Ikumbukwe mwezi uliopita Harmonize alitoa wimbo uitwao ‘Niambie’ lakini inavyoonekana wimbo huo haujawa na nguvu kubwa mtaani na hata katika vyombo vya habari kama ilivyokuwa kwa nyimbo zake tatu za mwanzo.
Kwa akili ya kawaida tu ili kujinasua katika hilo ndipo akamua kudondosha ngoma nyingine kwa ‘hasira’ na kuamini msanii kutoka WCB pekee ndiye anaweza kurudisha ushawishi wake unaotaka kufifia, je mbeleko hii itafaikiwa? Naomba nikuache tukutane wiki ijayo.
Kwa maoni 0755 299596

0 Comments:
Post a Comment