Saturday, July 22, 2017

Msanii msomi Nollywood afunguka

MSANII anayekuja kwa kasi katika filamu za Nigeria, Jemima Osunde ambaye anacheza kama Leila katika tamthilia ya Shuga inayorushwa na MTV TV, pia anasomea udaktari.
Mwanadada huyo ambaye anaendelea vizuri na masomo huku akiwa mwanamitindo na msanii, atakuwa miongoni mwa washiriki katika sehemu ya sita na saba katika tamthilia ya Shuga ambayo inaandaliwa nchini hapa.
Katika mahojiano yake hivi karibuni, Osunde aliweka wazi kwamba masomo yake ndicho kitu anachokipa kipaumbele ikifuatiwa na usanii.
Alisema yupo makini ndio maana hachanganyi kazi anayofanya ya usanii na masomo yake.
“Ninajiwekea ratiba ngumu kwa uangalifu ili niweze kufanya mambo yangu, nina mipango mizuri ndio maana sishindwi kufanikiwa. Upendo na furaha ninayoipata inakuja kwakuwa nafanya vitu ninavyovipenda,” alisema.

0 Comments: