Saturday, June 24, 2017

Vanessa Mdee amtumia ujumbe Jux


MSANII Vanessa Mdee Juni 22, mwaka huu ameamua kutuma ujumbe baada ya maswali ya watu mbali waliokuwa wanahoji kitu alichokuwa anafanya Jux China.
Vanessa ameamua kueleza wazi kuwa kile ambacho watu walitaka kufahamu kuhusu Jux ambaye ndio mpenzi wake ni kwamba alikuwa anakwenda China kwasababu alikuwa masomoni na sasa amehitimu Degree ya Computer Science kutoka Guangdong University kilichopo China .
Jux kuonesha picha hizo kupitia Instagram yake kumewafanya watu wengi watoe pongezi kwake na miongoni mwao ni Vanessa Mdee aliyetumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea hisia zake.
Jux ameamua kuweka picha za matukio mbalimbali yanayoonesha mahafali yake ambapo Vanessa akaamua kuandika “ Hapo watu walikuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii picha jibu la kutosha. Umeweza kufanya yote, muziki, biashara na shule. Muda wa vibunda babaaa.”

0 Comments: