Saturday, June 3, 2017

Mercy Johnson ‘atoka povu’ mtandaoni

MSANII nguli wa filamu Nigeria, Mercy Johnson amejikuta akimwita shabiki wake mjinga baada ya kuitwa Juliet Ibrahim ambaye alishindwa kwenda kanisani.
Tukio hilo ambalo halikutarajiwa kutokea, lilitokea siku chache zilizopita katika ukurasa wa Instagram wa mwanadada huyo ambapo alionesha kukosa uvumilivu naye.
Mercy ambaye ni mama wa watoto watatu alikosana na Juliet katika kampeni ya GLO kitu ambacho kilisababisha Juliet asiende kanisani kwasababu ya hilo.
Mwanadada huyo alitakiwa kumuacha Juliet aendelea kuelezea kinachoendelea kwa shabiki wake lakini ilishindikana kwa kuingilia kati na kumuita shabiki mjinga.


0 Comments: