MSHANGAO mkubwa ulinikumbuka wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akijibu hoja ya Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule kuhusu unyanyaswaji wanaofanyiwa wasanii wanaoimba nyimbo za kuiponda Serikali.
Sauti ya Mwakyembe iliyokuwa ikitoa majibu yale ndio iliyonichanganya na kujiuliza kama kweli Waziri anajua kazi za Muziki ni nini?
Kwa ufupi tu Muziki kazi zake kubwa ni kuelimisha na kuburudisha, kuelimisha jamii pale inapokosea lakini pia kuwapa burudani pale wanapokuwa wakiihitaji.
Na kwa maana hiyo hapo ndipo ule msemo wa Msanii ni Kioo cha Jamii unapotumika.
Kama Serikali au jamii inafanya mambo mabovu halafu Wasanii wanakaa kimya bila kutunga nyimbo za kukosoa kuna maana gani ya kuwa na wasanii nchini kwetu?
Kauli ya kwamba wasanii hawapaswi kuimba Siasa ni kauli nyepesi ambayo nimewahi kuisikia ikitoka kinywani kwa Waziri mwenye dhamana ya Sanaa.
NAMSAHIHISHA KUHUSU FELLA KUTI
Wakati akitoa kauli hiyo ya kuwataka wasanii kuacha kuimba nyimbo za Siasa, Dk Mwakyembe alisema ametembelea Nchi nyingi na hakuna hata mojawapo ambayo Mwanamuziki/Msanii aliyeimba nyimbo za kuikosoa Serikali alifanikiwa.
Kosa la kwanza kufanywa na Dk Mwakyembe ni kuamini wasanii wakiimba nyimbo zenye maudhui ya Siasa zinakuwa zinaiponda Serikali, la hasha anakosea sana bali zinakuwa ni nyimbo za kuikosoa Serikali pale inapokosea.
Na Msanii kama Mtanzania yoyote anaweza kutunga wimbo wa kuikosoa Serikali pale anapoona imefanya sivyo ndivyo bila kubugudhiwa wala kutishiwa usalama wake.
Haki ya mtu kuzungumza na kutoa maoni yake bila kuvunja sheria iko wapi kama wasanii wanakatazwa kutunga nyimbo za kuikosoa Serikali? Makosa makubwa kuwahi kufanywa na Waziri mwenye dhamana ya Tasnia nchini.
Tukirudi katika mfano wake kuhusu Fella Anikulapo Kuti (Hayati) ambaye alikuwa Mwanamuziki nchini Nigeria, Dk Mwakyembe anasema Fella aliishia pabaya kutokana na tungo zake za kuiponda Serikali (ingawa hakua anaponda alikuwa akikosoa).
Halafu anasema kwamba wasanii kama Diamond, Ali Kiba, P Square na Chameleone wamefanikiwa kwa sababu hawaimbi nyimbo za Siasa.
Ambacho Dk Mwakyembe anashindwa kuelewa ni kwamba Fella Kuti yeye aliitengeneza Historia yake kwa namna ya kipekee na kamwe hatokaa apotee katika historia ya Nigeria.
Alitengeneza jina lake kama msanii mkubwa aliyepata mafanikio makubwa ikiwemo kuufikisha muziki wake hadi nchini Marekani ambapo jina lake la Ransome lilipozaliwa.
Lakini pia akajenga jina lake kama Raia wa Nigeria ambaye alipigania maslahi ya Nchi yake na wananchi wenzake waliokuwa wakiteswa na utawala uliogubikwa na rushwa na ufisadi.
Fella Kuti alifungwa jela mara kadhaa lakini bado hakusita kutunga rekodi za kuikosoa Serikali yake pale aliporudi uraiani.
Fella hakuwa muoga kukosoa, alikuwa jasiri na leo mitandao mbalimbali inamtaja kama msanii ambaye alitumia kipaji chake kuikomboa Nchi yake katika utawala wa Rushwa na Ufisadi.
Aliteswa, alinyanyaswa, aliharibiwa mali zake tu kwa sababu alitumia kipaji chake kuitetea Nigeria Nchi ya Mama yake. Uoga haukuwahi kuwepo moyoni mwa Fella Anikulapo Kuti.
Ataendelea kuwemo katika historia ya Nigeria na Afrika kwa ujumla, ‘legacy’ yake itadumu vizazi na vizazi.
Hajaacha urithi wa kuwa Mwanamuziki wa kubadilisha wanawake na kufanya starehe kwa kigezo cha umaarufu wake kama wasanii ambao Dk Mwakyembe anatutajia.
Amekufa akiacha alama ya kuwa mpigania haki jasiri.
DIAMOND HAFANYI SIASA?
Nilicheka wakati Dk Mwakyembe akimtaja Diamond na wenzake kama msanii aliyefanikiwa kimuziki bila kufanya siasa, nilicheka sana, tena nikacheka kwa nguvu.
Diamond hafanyi siasa? Dk Mwakyembe ni kweli unayozungumza au umesahau?
Ngoja tuchukulie umesahau na tukukumbushe, hivi Waziri umesahau kuwa Diamond na kundi kubwa la wasanii wenzake mlilitumia katika majukwaa yenu ya kisiasa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, 2015?
Umesahau kuwa huyo Diamond ambaye eti unajaribu kumfananisha na Fella Kuti alibadilisha baadhi ya nyimbo zake ikwemo ule wa Number One na kuutungia mashairi ya Siasa ya kukisifia Chama chako, 2015? Umesahau?
Umesahau kuhusu kampeni ya Mama na Mtoto iliyoendeshwa na kuratibiwa na wasanii wa Filamu wakiongozwa na Wema Sepetu na Steve Nyerere chini ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu? Labda umesahau.
Labda unataka kutuamisha kuwa msanii mzuri ni yule anaeitunga nyimbo za kuisifia Serikali tu, kama hiyo ndio tafsiri yako basi Dk unakosea kwani rafiki bora hawezi kukusifia kila siku, inampasa kukukosoa pia siku ukiteleza.
UNAIJUA THAMANI YA MUZIKI?
Kabla ya ujio wa muziki huu wa Bongo Fleva ambao uliletwa kwa madhumuni ya kuiangamiza Muziki wa Hip Hop (nitakuja kueleza siku nyingine kuhusu hili) ni Hip Hop ambayo ilikuwa ikitamba.
Hip Hop ni muziki ambao ulianza miaka ya 1970 katika eneo la Bronx jijini New York kama harakati za kuwakomboa wa-Marekani weusi na watu jamii ya wa-Latin ambao walikuwa wakibaguliwa na Wazungu.
Ghetto Brothers, Puerto Rican na akina DJ Kool Herc ni baadhi ya wanamuziki ambao walitunga nyimbo nyingi za kuwakomboa watu weusi kutoka kwenye ubaguzi wa rangi na kuwafanya wathaminiwe.
Tunapozungumza leo Hip Hop ndio muziki ambao umeyafanya maisha ya vijana wengi wenye mafanikio duniani kote kufanikiwa na hata katika listi ya wasanii wenye mpunga mrefu majina ya wakali wa RAP yapo katika namba za juu.
Nikukumbushe huu ndio muziki ambao ulipambania haki ya mtu mweusi, muziki ambao ulipambana na ubaguzi wa rangi huku ukikosoa Serikali.
Hivyo muziki una nguvu katika kurekebisha mambo ambayo hayaendi vizuri iwe Serikalini au uraiani. Wanamuziki hawapaswi kupangiwa vitu vya kuimba na kuandika ‘as long as’ hawavunji sheria za Nchi.
UMESAHAU MAFANIKIO YA JAY, SUGU?
Kama Dk Mwakyembe ulidhani mafanikio ya muziki ni kuwa na mali nyingi pekee basi unakosea sana, muziki wa kuwatetea wanyonge, kuikosoa Serikali na wanasiasa ndio umewafanya leo Sugu na Profesa Jay kukunja suti zao bungeni.
Sugu ndie muasisi wa Hip Hop nchini muziki, nyimbo zake zilizojaa maudhui ya kukosoa, kuelimisha ndio zimempa mafanikio makubwa ikiwemo kuwa Mbunge aliyepigiwa kura nyingi kipindi cha kampeni (MVP).
Tungo za Profesa Jay ziliwashawishi vijana wengi kuingia katika muziki kutokana na kujaa maudhui ya kuelimisha, kukosoa serikali na wanasiasa kwa ujumla.
Ni dhambi kubwa kupangia wasanii kitu cha kuandika na kuimba maana wana nafasi kubwa katika kuijenga Nchi kupitia nyimbo zao.
Bob Marley mkali wa Muziki wa Reggae duniani aliwahi kutunga wimbo wa Africa Unit ambao aliutumbuiza katika sherehe za Uhuru wa Zimbabwe na kuwanyanyua vitini viongozi wakubwa wa Nchi za Kiafrika waliohudhuria.
Bob anakumbukwa duniani kote kwa namna ambavyo alitumia mashairi yake kutangaza amani na kupigania ukombozi wa mtu mweusi, leo hii sisi tunaambiwa wasanii wasiikosoe Serikali.
Roma Mkatoliki alisifika kwa uwezo wake wa kutungo nyimbo za kukosoa na kuelimisha kiasi kwamba Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete aliwahi kumuita Ikulu. Siasa na muziki haviwezi kuwekwa mbali.
Charles James
Kwa maoni 0713 153035

0 Comments:
Post a Comment