MUZIKI wa Bongo Fleva unazidi kubadilika kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, kila siku ni mapinduzi katika muziki huu.
Mabadiliko katika sekta yoyote hayawezi kuepukika, endapo utajitenga na hilo kupata mafanikio ni vigumu, kwani madiliko huambatana na mabadiliko.
Tumeshuhudia mabadiliko na mapinduzi makubwa katika bongo fleva, wanamuziki wamepata nafasi za uongozi katika ubunge na udiwani.
Kwa mara ya kwanza 2010 Joseph Mbilinyi ‘Mr Two Sugu’ anapata nafasi ya kuingia bungeni kupitia kura za wananchi wa Mbeya Mjini.
Kama haitoshi 2015 anatetea nafasi yake. Bongo Fleva inazidi kupata heshima baada ya Joseph Haule ‘Prof Jay’ kuingia bungeni mwaka huo kwa wingi wa kura za wananchi wa Mikumi.
Azma, Mr Blue na Sholo Mwamba
Hawa ni wasani watatu tofauti kabisa, Mr Blue akifanya muziki wa rap toka kitambo, huku Sholo Mwamba akiibuka hivi karibuni kupita muziki wa Singeli na Azma akifanya muziki wa Hip Hop.
Hawa ndio wasanii pekee waliopata nafasi ya kufanya kolabo na hawa wabunge (Sugu na Prof Jay) baada ya kumalizika uchaguzi wa mwaka 2015.
Leo katika zeze kolabo ningependa tuziangalie na kuzichambua kazi hizi mbili walizofanya pamoja.
Freedom - Mr Two Sugu
Huu wimbo ulifanyika MJ Records kwa prodyuza Marco Chali, mwanzoni wimbo huu ulitambulika kama wa Mr Blue lakini baadae ukaja kuwa wa Sugu, hilo tuliache kwanza.
Katika wimbo huu Sugu ameeleza alivyokwenda nje ya nchi kutafuta maisha na hata aliporejea Tanzania bado maisha yake yalisalia kuwa yale yale yasiyo na makuu.
Kazi kazi - Prof Jay
Baada ya kupata ubunge watu wengi walikuwa na shahuku ya kujua kama Prof Jay ataendelea kufanya aina yake muziki kwa kuachia nyimbo kama Ndio Mzee, kikao cha Zarura na Nang’atuka.
Kinyume na matarajio ya weingi Prof Jay akaja na muziki wa singeli. Licha ya kuwepo wasanii wengi wanaofanya vizuri kwenye singeli, ila jicho la Prof Jay alilidondoka kwa Sholo Mwamba.
Ndipo wimbo huu ukatoka, wapo waliokubali na wapo ambao hawakuridhika, unajua kwa nini, sababu inakuja.
‘Povu’ kwa sugu
Tukianza na Freedom, awali ilitambulika wimbo huu ni wa Mr Blue lakini video yake ilipotoka hakuwepo Mr Blue kitu kilichomfanya kulalamika kuwa ameporwa wimbo wake.
Video aliyotoa Sugu aliifanyika kwa ‘Director’ Hanscana. Ndipo rapa Ney Wa Mitego alipoamua kuingilia ugomvi huo kwa kusema.
“Blue angekuwa ni mshikaji wangu ningemshauri amtoe Sugu, kama inawezekana aniweke mimi kwenye ‘chorus’ tuharibu hali ya hewa tutajuana huko mbele ya safari, kama ni hela ya kuifanyia Video ya ngoma hii mimi nitalipa hata kwa GodFather au Hanscana”. Alisema Ney wa Mitego.
Lakini baadae baadae prodyuza Marco Chali alisema mdundo wa wimbo ulitengezwa na mdogo wake, Daxo Chali ukiwa na ‘chorus’ tayari na ulikuwa ikisubiri mtu wa kuingiza ‘Verse’ tu.
Aliongeza kuwa Mr Blue alipewa mdundo na kuamua kumshikisha Sugu, lakini hakutilia mkozo katika wimbo, ndipo Sugu alipoamua kuufanya upya pamoja na video bila Mr Blue kujua.
Marco Chali alisema wote wawili hawakulipia wimbo huo na MJ Records iliwapa bure tu, hivyo anashangaa kuona Mr Blue analalamika. Uzuri ni kwamba suala hilo limeshazungumzwa na kumalizika.
Garagasha - Azma
Jina kamili anajulikana kama Azma Mponda ni mwanamuziki wa Hipo Hop toka mkoani Mbeya lakini mara nyingi amekuwa akifanya baadhi ya kazi zake nchini Kenya ambako alisoma.
Mwaka huu ametoa wimbo uitwao Garagasha ambao ameshirikisha kundi la The Amazing ambalo linaoundwa na Izzo Buziness na Abela, bila kumsahau Sugu. Azma alisema wimbo huu ulilenga kuwashirikisha wasanii kutoka mkoani Mbeya tu ndio maana alifanya hivyo licha ya kuwa na mipango ya kufanya na wasanii wengine.
Twende mbele nyuma, Mr Blue na Sholo Mwamba ndio wasanii pekee waliopewa shavu na wabunge hawa tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka jana, huku Azma akimshirikisha Sugu kama nilivyoeleza.
Peter Akaro
Kwa maoni 0755 299 596

0 Comments:
Post a Comment