NYOTA wa Kiwanda cha Filamu cha Nollywood, Bewaji Folashade, yupo katika wakati mgumu baada ya kunusurika kutekwa na watu wasiojulikana mjini Ibadan.
Mwanadada huyo alitokewa na tukio hilo wakati akirudi kufanya filamu Akobo karibu na Ibadan na kusema alitekwa na wanaume wawili waliokuwa katika pikipiki mtaa wa Adeyemi.
Katika taarifa yake, msanii huyo alisema, wamaume hao walimpeleka sehemu ambayo haifahamu na kuanza kuhangaika kujiondoa mikononi mwao.
Alisema ni kaka angezembea wangemuua na watu wasingeona mwili wake kwani alipata mateso wakati wakimchukua ila alipambana nao hadi pikipiki kuanguka huku akipiga kelele lakini anashukuru alikuja kuokolewa.
0 Comments:
Post a Comment