MKALI wa filamu za Nollywood, Halima Abubakar, ambaye amerejea hivi karibuni nchini kutoka India alikokwenda kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe tumboni, amekana madai yaliyozagaa mitandaoni kwamba anaumwa saratani.
Mara baada ya kurejea akiwa mzima wa afya njema, staa huyo wa filamu alitaka kuombwa msamaha na yeyote au kikundi cha watu kilichoeneza tetesi hizo kuwa anasumbuliwa na saratani.
“Yeyote au kikundi chochote cha watu kilichotunga na kusambaza habari hizo, tafadhali waje au aje aniombe msamaha kwani, habari hizo zimeniumiza kwa kiasi kikubwa. Huwezi ukamzushia mtu kuwa ana saratani wakati alikuwa ana uvimbe kwenye kizazi” alisema Halima.
Halima ambaye kwa sasa amenyoa nywele zake kutokana na makali ya dawa alizokuwa akizitumia, aliandika maneno hayo kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram na kueleza kuwa Naijagist ambao waliandika habari hizo wamwombe msamaha haraka.

0 Comments:
Post a Comment