Saturday, May 27, 2017

Mwasit achanga fedha kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto


MSANII wa Bongo Fleva Mwasit Almas ameamua kutoa fedha kwa ajili ya kuchangia upasuaji wa moyo kwa mtoto mmoja kati ya watoto 100 wenye uhitaji wa kufanyiwa upasuaji huo.
Mwasit ametoa ahadi hiyo Dar es Salaam jana wakati  Clouds Media Group walipoamua kufanya harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia watoto hao ambao matatizo ya moyo waliyonayo yamewafanya kupoteza tabasamu.
“Binafsi nitatoa fedha kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mtoto mmoja, najua matatizo waliyonayo yanawanyima furaha watoto wenyewe, wazazi na Watanzania kwa ujumla.
“Hivyo lazima niwe miongoni mwa walioguswa kwa vitendo, hivyo naahidi kuchanga fedha kwa ajili ya kufanikisha upasuaji huo kwa mtoto mmoja ingawa najua nina marafiki wengi iwapo watachanga fedha tutaangalia kama tutaweza kusaidia mtoto mwingine,”anasema Mwasit.


0 Comments: