Saturday, May 20, 2017

Moji Olaiya afariki dunia


MSANII wa filamu za Nollywood, Moji Olaiya, 42 amefariki Dunia juzi baada ya  kujifungua kwa shida akiwa hospitalini nchini Canada.
Kifo cha msanii huyo ni pigo kwa Nollywood kutokana na umuhimu wake wake hasa katika filamu za Yoruba.
Moji ambaye alimkaribisha mtoto wake mpya Machi, mwaka huu, alifariki juzi usiku nchini humo.Taarifa zilieleza alifariki baada ya kupata ugonjwa wa shambulio la moyo.
Tasnia hiyo imekuwa kwenye huzuni mkubwa tangu kufariki kwa mwanamama huyo ambaye alikuwa na msaada mkubwa ka wasanii wanaochipukia.


0 Comments: