Monday, May 8, 2017

Maproduza watano Bongo waliopewa ‘shavu’ na wasanii

KAZI ya prodyuza anapokuwa studio na msanii ni kurekodi, kumtengenezea mdundo mzuri na kumpa msanii maelezo juu ya kitu wanachoenda kukifanya. Lakini vipi pale prodyuza anapofanya kazi yake kwa ubora kisha anashirikishwa katika ile kazi alikuwa akiisimamia?
Najua hujanielewa, simaanishi prodyuza aliyetengeneza wimbo wake binafasi, bali aliyeshirikishwa kwenye kazi a
Leo kupitia mtandao Zeze Kolabo nakuletea maproduza watano waliokumbana na bahati hiyo.
 P Fank Majani 

Ni prodyuza aliyedumu kwa kipindi kirefu katika muziki wa Bongo Fleva na ameutoa mbali hadi hapa ulipo kwa sasa.
Bado anahudumu katika studio za Bongo Records na mara kadhaa amekuwa akisikika kupitia kazi za wasanii wachache anaofanya nao kazi kwa sasa ukilinganisha na hapo awali.
Kwenye ngoma ya Madee ya ‘Yote Maisha’ aliyoitengeneza zaidi ya miaka 10 iliyopita, sauti ya P Fank inasikika katika kiitikio cha ngoma hiyo na hata ngoma hiyi inapoanza (intro) na mwisho (outro).
P Fank alitumbukiza tena sauti yake katika ngoma ya Jay Moe ulikwenda kwa jina la ‘Famous’, ngoma hiyo ilimrudisha Jay Moe kwenye muziki kwa kipindi kile mara baada ya ukimya wa muda mrefu. 
Marco Chali

Ni prodyuza anae fanya kazi zake katika studio za MJ Records kwa muda sana, vile vile ni mshindi wa tuzo ya KTMA kwa mwaka 2008.
Amekuwa akishirikiana na ndugu zake, yaani Bifuchaa, Zachaa na Daxo Chalii kufanya kazi nzuri zenye ubora. Sauti yake imesikika kwenye ngoma za wasanii wengi kidogo.
Rapa Godzilla amekuwa na bahati ya kunasa sauti ya Marco Chalii mara kwa mara, kwa mara ya kwanza kwenye ngoma ya King Zilla, sauti ya Marco inasikika kwenye kiitikio.
Ngoma ya pili ni ‘Nataka’ ambayo ulikuwa katika maad
Quick Rocka katika ngoma yake ya ‘My Life’, sauti ya Marco Chali inasikika kwenye kiitikio na mwishoni mwa ngoma hiyo.
Prof Jay nae hakuwa nyuma kuinasa sauti ya prodyuza huyo kwani alifanya hivyo kwenye ngoma yake ya ‘Kamili Gado’, Marco alisikika mwanzo mwisho.
 Dunga 


Jamaa anatokea nchini Kenya na alipokuja Bongo alileta utofauti katika muziki wetu.  Aliyeleta muziki wa ‘Bounce’, ni aina ya muziki ulipendwa sana kipindi cha nyuma, wasanii kama JCB, Noorah na Black Ryno walishafanya aina hiyo ya muziki.
Joh Makini ameshainasa mara tatu sauti ya Dunga aliyekuwa akisimamia lebo ya Mandugu Digital. Kwa mara kwanza Joh Makini alimshirisha Dunga katika ngoma yake ya ‘Chochote Popote’ iliyotoka mwaka 2006.
Kisha kufuatia na ngoma kama ‘Manuva’ na ‘Sijutii’, zote Dunga amesikika vema kwenye kiitikio, huku wakipokezana na Joh Makini.
 Man Water 

Anafanya kazi zake katika studio za Combination Sound, na pia ni mshindi wa KTMA kwa mwaka 2013 kama prodyuza bora wa mwaka.
Ni mkali wa ‘back vocal’ huwa hakosei katika hili, alishafanya hivyo kwenye ngoma ya Alikiba ‘Dushelele’ na ngoma ya mwanadada Lady Jaydee ‘Yahaya’.
Mr Blue nae hakuwa nyuma kuipata sauti ya Man Water, hilo lilifanikiwa katika ngoma yake ya ‘Nipende Kama Nilivyo’.
 Fundi Samweli
Ni prodyuza kutoka nchini Sweden na alikuja hapa Bongo na aina yake ya  muziki yenye vionjo ambayo havikuzoelekeka hapo awali.
Aliingiza sauti yake kwenye  ngoma ya Joh Makini ya ‘Nikumbatie’ ambayo ilifanya vizuri kwa kiasi kikubwa.
Haikuishia hapo kwani alifanya hivyo tena kwenye ngoma ya  Nako 2 Nako Soldiers ilikwenda kwa jina la ‘Sweet Sixteen’ iliyotoka mwaka 2011.
Pia alifanya ‘back vocal’ kwenye ngoma ya Linex’ Ifola’, vile vile mwaka jana alipewa shavu na msanii Marlaw kwenye ngoma itwayo‘Pamoja’.


Peter Akaro
Kwa maoni ushauri 0755 299596

0 Comments: