MAISHA ya kufanya kazi kama Kundi au Timu yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana, ni moja kati ya maisha yenye changamoto nyingi kwa kila ambaye anakuwepo ndani ya kundi hilo.
Wapo wasanii wengi ambao kipindi wanatoka walianza kama kundi wakishirikiana katika kila hali huku wakiwa na lengo moja tu, ‘tukazeni wanangu faida ipo mbele siku tukitoka’.
Wote mnakua na kauli moja ya kishujaa, kauli ya kundi na Timu kwa ujumla kauli ya kushikamana ili kuweza kufikia pesa nyingi ambazo Joh Makin katika moja ya rekodi zake alituambie ziko mwishoni na ni ngumu kuzifikia.
Makundi mengi ya Wasafi wa Muziki yameshindwa kudumu, hii ni kwa sababu watu walidhulumiana, walinyimana nafasi au wengine kukosa uvumilivu kama nilivyoeleza hapo juu kuwa unahitajika sana.
Katika makundi ambayo yana kiongozi baadhi ya wasanii huhisi wenzao wanapendelewa na hivyo huamua kujitoa, makundi yana changamoto aisee!
TMK Wanaume Family lilivunjika, East Coast Team walizinguana, Nako 2 Nako walimeguka, TNG Squad nao wakatifuana, makundi mengi yalishindwa kudumu, usisahau kuhusu Tip Top Connection nalo kwa myakati tofauti wasanii wake wamekuwa wakijitoa na kwenda kujitegemea.
Q BOY NA KISANGA CHA WCB
Ijumaa iiyopita nilikuwa namtizama ‘Stylish’ wa Msanii Diamond Platnumz, Q Boy Msafi akimwaga povu katika kipindi cha Shilawadu kinachorushwa na Clouds TV, kuhusu yeye kuondoka katika Lebo ya Wasafi inayomilikiwa na msanii huyo.
Kwa mujibu wa maelezo yake Q Boy anaeleza kuwa yeye na Diamond wamejuana na kuanza kufanya kazi mwaka 2010 na wala hawakuwahi kuingia makubaliano yoyote ya kimkataba kwa maana ya kulipwa kutokana na yeye kuhusika kama kinyozi na mtu anaesimamia suala zima la mavazi la Staa huyo ‘Stylish’.
Q Boy anasema walikuwa wakifanya kazi kama washikaji ambao waliamini siku moja watakuja kula vinono.
Nilijaribu kumsikiliza vizuri Q Boy ili nione kama kuna sehemu yoyote atamrushia makombora ya kumlaumu, Diamond lakini haikua hivyo badala yake alikuwa akionekana kumshambulia mmoja wa Meneja wa Lebo hiyo, Salaam SK.
Q Boy anasema tangu kutua kwa Salaam ndani ya WCB, yeye amekuwa akibaniwa huku nafasi yake katika kufanya maamuzi ikionekana kupungua. Alienda mbali zaidi baada ya kusema kuwa ilifikia hatua Salam aliagiza atolewe kwenye Kundi la Whatsapp la WCB.
Kwa muktadha huu inamaana Q Boy amejitoa WCB kwa kushindwa kuvumilia hali iliyopo baada ya ujio wa Salam. Sababu zile zile nilizozitaja za watu kujitoa kwenye makundi zikatolewa na Q Boy ikiwemo ya upendeleo kwa baadhi ya Wasanii.
SALLAM SK NDIO MBUZI WA KAFARA?
Hili ni la ngapi kulisikia kuhusu Sallam SK? Oktoba,
Kiba mwenyewe alimtuhumu Meneja huyo wa Diamond kuhusika na uzimaji huo kwa kuwa alikuwa nyuma ya Steji, ingawa baadaye Sallam alikanusha kuhusika na tukio hilo.
Tukio hilo lilizusha mjadala mkubwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii huku mashabiki wa pande zote mbili za Diamond na Kiba zikishambuliana lakini mwishoe tukio hilo lilipita.
Hivi karibuni tena kuliibuka mtifuano mitandaoni baina ya Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo akiwatuhumu mameneja wa Diamond, huku akimtaja Sallam na Babu Tale kuwa wanachangia kuharibu jina la Staa huyo na endapo hatochukua hatua dhidi yao watamshusha kisanii.
Ukijumlisha tukio la kwanza kule Kenya na hili la pili dhidi ya Shigongo kisha ukaja kuongeza hizi shutuma ambazo Q Boy amezitoa utaona kwamba Sallam anatumika kama Mbuzi wa kafara wa WCB.
Kama tuhuma zinatolewa na mmoja wenu ndani ya Kampuni alafu Kampuni ikakaa kimya maana yake mnamuunga mkono hivyo inawezekana Sallam akawa anatumika kama mbeba lawama wa WCB.
Ndio maana Diamond mwenyewe kama Bosi wa Lebo hiyo hajaongea chochote kuhusu Q Boy, Babu Tale wala Said Fella hawajazungumza maana yake wamebariki kila kinachoendelea.
HATA MBELE IPO HII
Mwanafalsafa maarufu nchini India, Mahatma Gandhi aliwahi kusema ‘The Only person to trust it’s you’ akimaanisha mtu pekee wa kumuamini ni wewe mwenyewe. Kule Marekani, Rapa Lil Wayne alimuamini Bosi na Mlezi wake kutoka Lebo ya Cash Money, Birdman kwa jinsi walivyoishi pamoja vizuri wakipambana kusaka noti na kuikuza lebo yao hiyo ambayo baadaye ilizaa lebo nyingine ya Young Money. Zaidi ya miaka 20 waliishi pamoja (kumbuka Birdman alimuokota Wayne na kumlea) lakini mwishoni mwa mwaka 2015 wakaanza kuingia katika mtifuano.
Wakati Wayne akidai Kampuni inambania kuachia Santuri (albamu) yake ya CARTER V, Birdman yeye alionekana wala hajali kuhusu Wayne zaidi alikuwa bize kuhakikisha anampromoti Rapa, Young Thug akiwa na lengo la kumfanya achukue nafasi ya Wayne. Ukiangalia stori ya Birdman na Wayne ambao wametoka mbali kabla ya kuja kuzinguana kutokana na kila mmoja kusimamia maslahi yake.
Wayne mwenyewe alikuwa akilalamika kuminywa ndani ya Kampuni huku Young Thug akipendelewa utaona haina utofauti nay a Q Boy kusema anaminywa, hasikilizwi na kuna wenzake wanapendelewa ndani ya Kampuni hiyo. Kama ilivyo kwa Q Boy ambaye amejitoa WCB na sasa anaonekana kubang na Young Dee, Wayne yeye ameondoka Cash Money na kujiunga na Lebo ya Roc Nation inayomilikiwa na Jay Z. Watu wanazima umeme tu.
Na Charles James
0 Comments:
Post a Comment