Tuesday, May 16, 2017

Bongo Fleva na ‘kampa, kampa tena’


 Izzo Buziness
LEO katika Zeze Kolabo nakuletea wasanii kadhaa wa Bongo Fleva waliofanya kazi zaidi ya moja, yaani msanii kamshirisha mwenzake kwenye ngoma yake, kisha baadae akaja kushirikisha msanii huyo huyo ila kwenye ngoma nyingine.
Kwa lugha isiyo rasmi ya mtaani tunasema ‘kampa, kampa tena’, ila hawa ni wale wasanii wasio katika kundi moja la kimuziki, lebo au umoja wowote. Twendwe tukawatazame.
Nay wa Mitego na Diamond Platnumz
Nay Wamitego alimshirikisha mkali huyu kutoka WCB kwenye ngoma yake ya ‘Muziki gani’ ambayo ilifanya vizuri sana na kumuongezea Nay wa Mitego mashabiki wengi.
Nay wa Mitego akaona isiwe tabu, akaja kumshikisha tena Diamond kwenye ngoma yake ya ‘Mapenzi au Pesa’ ambayo nayo ilifanya vizuri kwa kiasi fulani.
Izzo Buziness na G Nako
Mkali huyu wa hip hop kutoka Mbeya alimpa shavu G Nako toka kundi la Weusi kwenye ngoma yake ya ‘Walalahoi’ iliyotoka mwaka 2014.
Izzo akatambua bado uwezo wa G Nako unahitajika kwenye ngoma zake, ndipo alipofanya nae kazi nyingine itwayo ‘Shem Lake’ ambayo pia alikuwepo Mwana FA.
Damian Soul na Joh Makini
Mkali huyu ambae anaaminika kuwa na sauti ya kipekee sana kwenye Bongo Fleva alifanya kazi ya kwanza na Joh Makini iliyokwenda kwa jina la ‘Ni Penzi’ ambayo ilifanya jina Damian Soul kuwa kubwa.
Akamua kuchovia asali kwa mara ya pili kwa kumpa tena shavu Joh Makini kwenye ngoma yake ya ‘Baraka’ ilyopikwa na Pancho Latino pamoja na Hermy B kutoka Bíhits.
Shetta na Diamond Platnumz
Ngoma ya ‘Nidanganye’ waliofanya pamoja ilimpa jina kubwa na kumbadilisha kabisa Shetta kimuziki, achili hilo mbali pia ilimpa Shetta nafasi ya kuwania tuzo za KTMA kwa wakati ule.
Shetta alimua kufanya na Diamond kazi nyingine aliyoipa jina la ‘Kerewa’ lakini hii ilikuwa na utofauti kidogo na ile ya mwanzo, kwani aliwekeza fedha nyingi kwenye kuitangaza na ubora wa video.
Bill Nas na T.I.D
Hawa wote walikuwa wakifanya kazi chini ya usimamizi wa Radar Entertainment pamoja na Jordan na vipaji vingine.
Kolabo yao ya kwanza ni ile ijulikayo kama ‘Raha’ ambayo pia walimpa shavu Nazizi kutoka nchini Kenya.
Baada ya ngoma ya mwanzo kufanya vizuri Bill Nas alimpa shavu tena T.I.D kwenye ngoma  yake ya ‘Ligi Ndogo’, ni wazi na yeye alinogewa na kolabo dhidi ya mzee kigogo.
Izzo Buziness, Shaa  & Barnaba
Izzo aliwahi kuwakutanisha wakali hawa kwenye ngoma moja ambayo ilitamba sana kwenye Bongo Fleva, ngoma ni ‘Love Me’ ambayo mwishoni ndio inasikika sauti ya Shaa.
Achilia mbali kazi hiyo Izzo anakuja kufanya kazi nyingine na Shaa aliyoipa jina la ‘Kidawa’ ambayo nayo pia ilifanya vizuri. Izzo anaamua kuwakutanisha wote tena kwa pamoja kwenye ngoma yake ya ‘Usijioverdose’ ambayo pia ilifanya vizuri.
Linex, Diamond Platnumz
Kazi ya mwanzo waliifanya kitambo kidogo ambayo ni ‘Nitaificha Wapi’, kitambo hicho wote wawili muziki wao ulikuwa wa kiwango za kawaida ukilinganisha na sasa.
Wakati Diamond ameanza kupata mafanikio katika ngazi za kimtaifa, Linex aliona ni wakati muafaka wa kufanya kazi nyingine na Diamond kama njia ya yeye ‘kujipush’ kuelekea kimataifa zaidi.
Wakatoa kazi ya ‘Salima’ ambayo Linex aliamini ingemtangaza kimataifa, lakini utengenezaji wa video ilimkwamisha kitu kilicholeta mgogoro kati yake na director Adam Juma.
Country Boy na G Nako
Mkali  huyu wa kufanya cover ngoma za wasanii wa mbele alimpa shavu G Nako kwenye ngoma yake likwenda kwa jina la ‘Watch Me’.
Country Boy hakutosheka na kolabo hii, hivyo ya pili ikafuata kwa kuwa anajua sauti ya G Nako kwa sasa ni bidhaa inayouzika kirahisi kwenye soko la Bongo Fleva.
Kolabo ya pili ilikwenda kwa jina la ‘Mtaa Kwa Mtaa’ ambayo ilisumbua sana kwenye redio na mitaani, pamoja remix yake iliyowakutanisha wakali kibao kama Stamina na Chid Benz.
Tunda Man na Alikiba
Ni vigumu sana kwa wasanii wanaofanya muziki wa aina moja kufanya kazi kwa pamoja mara kwaa mara, hasa kwa wasanii wanaoimba ila hawa waliweza hilo.
Tunda Man alimshirikisha Alikiba kwenye ngoma yake ya ‘Starehe Gharama’ ambayo pia alikuwepo Chege mkali kutokaTMK, na huo ukawa mwanzo wa safari.
Safari ya kolabo ikaendelea, Tunda Man akuaja akampa tena shavu Alikiba kwenye ngoma ilyokwenda kwa jina la ‘Msambinunga’ iliyosimamiwa na prodyuza Shedy Clever.
Na Peter Akaro
Kwa maoni
0755 299596


0 Comments: