Sunday, April 2, 2017

Samkelo : Nipo tayari kupambana nao….


KISURA Samkelo Ndlovu ametangaza vita dhidi ya vidume ambavyo vimekuwa na tabia ya kubaka wanawake na kusema atahakikisha anatumia nguvu zake kupambana nao ili kukomesha tabia hiyo.
Alisema ni ujinga wanawake kuacha kuvaa nguo fupi au kutembea peke yao tu kwa sababu wanahofia kubakwa na wanaume wenye uchu wa ngono, na kutaka wanawake kushikamana kupinga udhalilishaji hyuo.

“ Binafsi sivai nguo fupi lakini bado pia haiingii akilini kwa wasichana kutoenda sehemu za kujirusha, kupanda teksi usiku peke yao eti kwa kuwa wana hofu na kubakwa, kama tusiposhikamana na kupinga uhuni huu kutakuwa hakuna maana ya kuishi,” anasema Samkelo.



0 Comments: