Hayan maneno ya Diamond kwenda kwa Ray C-
rayctanzania Mdogo wangu umenigusa sana nimetoa chozi, nashukuru sana kwa maneno yako ya faraja, Mungu ni mwema sana kwa kila jambo,maneno yako yamenipa nguvu na matumaini,Nashukuru sana sana 🙏🙏
- @Regrann from @diamondplatnumz - Salaam dada angu @rayctanzania
, siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi
unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa
Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali.... Nafarijika kuona wimbo
wako wa #Unanimaliza
watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni
miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya.... Ombi langu kwako
usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi
ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na
kumuomba Muumba, itapita....niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa
tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau
mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na
kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa
kwa mambo mbalimbali....InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi
zako na Maisha ya kila siku🙏 @rayctanzania - #regrann
0 Comments:
Post a Comment