Saturday, April 29, 2017

Aamua kufanya sherehe ya miaka mitano….

MUNGU mkubwa, Ni kauli yake Staa wa filamu Bollywood, Manisha Koirala baada ya kuviambia vyombo vya habari kwamba anatarajia kusherehekea miaka mitano ya uhai wake akiwa mgonjwa wa Kansa.
Mkali huyo aliyetamba katika filamu ya Subhash Ghai Saudagar amesema ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kuendelea kumpa pumzi licha ya kuwa na ugonjwa huo hatari ambao watu wengi wamekuwa wakiteseka nao na kupoteza maisha.
“ Nafikiri licha ya kusherehekea napaswa kutoa elimu kwa mashabiki zangu na kila mtu ili waweze kujua namna gani ya kupambana na Kansa, wengi wanauliza natumia nini lakini muhimu ni matumizi mazuri ya dawa (Kliniki) na mazoezi kama hamjui nafanya sana Yoga,” anasema Manisha.


0 Comments: