NI kama Ney wa Mitego ameanza kuwatahadharisha wasanii wenzake wa Bongo fleva wawe makini kwani kuna hatari ya muziki wao kupigwa mweleka na siasa.
‘Hitmaker’ huyo wa Wapo wimbo unaopendwa na Rais, John Magufuli, amesema watanzania kwa siku za hivi karibuni wametekwa na ombwe la Siasa hivyo wasanii wasipokuwa wabunifu wanaweza kujikuta muziki wao unadumbukia shimoni.
“Wasanii inabidi tupambane kuhakikisha tunaurudisha muziki wetu kwenye kilele chake, maana kila kona saa hivi ni siasa na kujua kiongozi gani ametoa tamko , hivyo tukomae kuirudisha Bongo Fleva yetu tofauti na hapo tutafia shimoni kama Bongo movie,”anasema Ney.
0 Comments:
Post a Comment