Friday, March 3, 2017

Pama D akanusha kujirusha kwa Mesen


HITMAKER wa kibao cha Daffa, Pam D ameweka wazi kuwa mahusiano pekee aliyonayo na Prodyuza Mesen Selekta ni wa kikazi na si kimapenzi kama ambavyo inavumishwa.
Mrembo huyo amekanusha taarifa hiyo kufuatia tetesi ambazo zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba anajirusha na Mesen huku akieleza kuwa wao ni marafiki ambao wanashirikiana kwenye kazi na hakuna la ziada.
Pam amesema pamoja na maneno hayo ambayo yamekuwa yakizagaa bado hatoacha kufanya kazi na Mesen ambaye wamekuwa wakitengeneza nae ngoma kali zinazojizolea umaarufu.
“ Unajua sisi wabongo tukiona watu wapo karibu tunaanza kuzusha ni wapenzi, sisi I washikaji ambao tunafanya kazi zetu pamoja, wenye mawazo kuwa sisi ni wapenzi wafute kwani wanajidanganya tu,” Anasema Pam D.

0 Comments: