Friday, March 3, 2017

Mwana FA asema TID atarejea kwenye afya yake


RAPA anaetamba na hit ya Dume Suruali, Mwana FA amefunguka kuhusu hali ya kiafya ya mkali wa Vocal, TID Mnyama baada ya kusema anaendelea vizuri na mazoezi na kwamba muda si mrefu atarudi kwenye hali yake ya kawaida.

TID ambaye alifunguka na kukiri kutumia madawa ya kulevya hivi karibuni, ameanza mazoezi ‘Gym’ ya kujiweka fiti na kurudisha mwili wake ambao ulikuwa umedhoofika kutokana na kutumia dawa hizo.
Sasa Mwana FA ambaye anafanya mazoezi na Mnyama kwenye Gym moja amefunguka kuwa mkali huyo amekuwa akijitahidi kufanya mazoezi kwa kasi na nguvu na anaamini baada ya muda mfupi atakuwa amerejea kwenye hali yake ya kawaida.
“ Unajua TID alikuwa anafanya mazoezi zamani ila kutokana na mitikasi ya hapa na pale akawa ameacha, kwa sasa anafanya mazoezi sana na hata ukija hapa Gym utakuta yeye ndie ameloa jasho kuliko wote hapa, naamini muda sio mrefu afya yake itaimarika,” Anasema Mwana FA.



0 Comments: