MREMBO anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini India ‘Bollywood’, Neha Dhupia amesanua kuwa kutoandikwa kwake ovyo kwenye vyombo vya habari ni kutokana na malezi bora aliyopewa na wazazi wake huku pia akiwa msiri na maisha yake.
Diva huyo anayetimiza muongo mmoja tangu aanze kuigiza anasema amekuwa akifanya mambo yake mengi kwa siri ili kulinda heshima yake mbele ya jamii ambayo imekuwa ikimtizama kama mwigizaji asiye na skendo Bollywood.
Neha anasema anafahamu ugumu wa tasnia ya filamu nchini humo ulivyo huku akifafanua kuendelea kwake kukaa kileleni kwa muda mrefu bila kuporomoka kutokana na kujituma katika kazi.Pia kuwa na marafiki ambao wanamshauri vizuri na wasio na skendo.
“Ni ngumu kukaa juu kama hujitumi kutoa kazi bora, ninatimiza miaka 10 katika gemu kwa sababu ya namna ambavyo nimekua nikijiheshimu na kutokuweka mambo yangu hadharani,”anasema.
Diva huyo anayetimiza muongo mmoja tangu aanze kuigiza anasema amekuwa akifanya mambo yake mengi kwa siri ili kulinda heshima yake mbele ya jamii ambayo imekuwa ikimtizama kama mwigizaji asiye na skendo Bollywood.
“Ni ngumu kukaa juu kama hujitumi kutoa kazi bora, ninatimiza miaka 10 katika gemu kwa sababu ya namna ambavyo nimekua nikijiheshimu na kutokuweka mambo yangu hadharani,”anasema.
0 Comments:
Post a Comment