Friday, February 17, 2017

Wema afurahi Manji kupata dhamana


MREMBO Wema Sepetu amefunguka na kueleza furaha yake iliyoambatana na kumshukuru Mungu baada ya Mahakama ya Kisutu kumwachia kwa dhamana Mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.

Wema ametumia akaunti yake ya Instagram kueleza Manji kupata dhamana ni jambo ambalo limempa faraja sana na kuongeza kuwa ni wakati wa kuendelea kumshukuru Mungu kwa mapenzi aliyoyaonesha.
“Mule ndani si kuzuri kabisa na anayekupeleka kule hawezi kuwa rafiki yako.Tena wakukaa naye mbali kabisa.Kama kawaida sitaki maoni”.
Maelezo hayo ya Wema yanakuja kipindi ambacho kuna Watanzania wengi ambao nao wamefurahishwa na dhamana aliyopewa Manji huku wakiendelea kumwombea kwa Mungu yaliyopo mbele yake yaishe ili maisha mengine yaendelee.


0 Comments: