Nairobi, Kenya
MSANII nyota wa muziki nchini Kenya, Jaguar ameiomba serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kutunga sheria kali zitakazolenga kupambana na vileo kwa madereva ili kupunguza ajali za barabarani.
Alisema kumekuwa na kesi kadhaa ambazo zinaonesha ajali zimesababishwa na ulevi wa madereva lakini sheria za nchi zimekuwa ni legelege kwa kiasi kikubwa ndiyo maana hayo yote yanatokea.
Aliongeza kwa kusema kuwa kama serikali kweli itaingia kwenye vita ya kupambana na ajali za barabarani basi moja ya mbinu yao kubwa wanayotakiwa kuitumia ni kutunga sheria mpya kuhusu vilezi hasa kwa madereva.
Nyota huyo wa muziki wa kizazi kipya anajulikana zaidi Afrika Mashariki baada ya kutamba na vibao vyake kadhaa kama vile Nimetoka Mbali, Kioo na Kipepeo.

0 Comments:
Post a Comment